Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi katika uchaguzi wa marudio katika kata ya Bugalama iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kwenye uchaguzi huo uliofanyika Agosti 12,2018,Vyama vitatu vilisimamisha wagombea katika kata hiyo na mgombea wa CCM Izengo Josephat alitangazwa mshindi kwa kura 2137 akiwashinda wapinzani wake Stephano Izengo wa CHADEMA kwa kura 571 huku mgombea wa ACT wazalendo Jilala Seni akipata kura 32.
Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika kufuatia aliyekuwa diwani wa CHADEMA Izengo Josephat kuhamia Chama Mha mapinduzi CCM na chama hicho kilimpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho.
Social Plugin