MAGUFULI : URAIS NI KAZI NGUMU

Rais John Magufuli amesema hakuna mwenye uhakika wa cheo katika serikali ya awamu ya tano hata yeye hana uhakika.


Ameyasema hayo leo Agosti Mosi, wakati akihutubia mara baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu.


Amesema kazi yake ni ngumu na wakati mwingine halali usiku au akaamshwa saa nane za usiku akipewa taarifa mbalimbali.


“Hii ni kazi ngumu, its terrible job, kama jana usiku nimeamka saa nane usiku IGP ananipigia simu anasema kuna watu wetu wamepata ajali mpakani, kuna mwingine anasema hivi. Basi na nyinyi mteseke kama mimi ninavyoteseka,” amesema

Amewaambia wateule hao hakuna anayeweza kukwepa kazi hiyo na ana uhakika wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia wananchi.

Na Elias Msuya, Mwananchi 

Theme images by rion819. Powered by Blogger.