Picha : JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOMPOKEA WAZIRI KIGWANGALLA UWANJA WA NDEGE DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara mara baada ya kuwasili kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa kwa ajili ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika  ajali ya gari mkoani Manyara.
Ndege maalumu iliyombeba Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere  kutokea mkoani Arusha majira ya jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alipata ajali ya gari mkoani Manyara.
PICHA NA IKULU

 Rais John Magufuli amempa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyepata ajali ya gari leo Jumamosi Agosti 4, 2018 mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema kiongozi mkuu huyo wa nchi amemuombea waziri huyo apone haraka na kuwashukuru madaktari na wauguzi wa kituo cha afya Magugu walioanza kumpa huduma ya kwanza.


Pia, amewashukuru viongozi wa hospitali ya Selian ya jijini Arusha kwa juhudi walizozifanya kuokoa maisha ya Dk Kigwangalla na majeruhi wengine wa ajali hiyo.

Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa familia, wafanyakazi wa wizara, ndugu, jamaa na marafiki wote kufuatia kifo cha ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa leo jioni Rais Magufuli aliungana na viongozi wa wizara hiyo kumpokea Dk Kigwangalla katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Dk Kigwangalla amesafirishwa kwa ndege kutoka Arusha kuja jijini hapa kwa matibabu zaidi.

Inaeleza kuwa waziri huyo amepata ajali katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu Wilaya ya Babati mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Temba huku watu wengine watano akiwemo yeye kuumia.


Akiwa JNIA, Rais Magufuli alikuwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527