MWANAFUNZI MATATANI KWA KUMKABA MAMA YAKE MZAZI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto

Mwanafunzi huyo anatuhumiwa kujiunga na kikundi cha uhalifu cha Kamchape ambacho kinajihusisha na ukabaji na uvunjaji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema kuwa kijana huyo amekuwa akijishughulisha na uhalifu ambapo kwa siku za hivi karibuni aliwahi kukiri kumkaba mama yake mzazi lakini mama huyo hakujua kuwa aliyemkaba ni mwanaye.

"Huyu kijana alijua kuwa aliyemkaba na kumpora ni mama yake mzazi, hivyo alivyogundua aliyempora ni mama yake alichofanya ni kumwachia mkoba aliompora na kutokomea kusikojulikana bila yule mama kufahamu, kuwa aliyemkaba ni mwanaye wa kumzaa", amesema Muroto

Aidha, Kamanda Muroto amesema baada ya tukio hilo kijana huyo aliachiwa lakini alikamatwa tena, alipobainika kuwa amehusika katika kuvunja nyumba ya mtu na kuwafunga kamba wenye nyumba ili wawaibie.

Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo amedai chanzo cha yeye kujihusisha na matukio hayo ya uhalifu ni kutokana na hali ngumu ya maisha ndio imemfanya kutenda hayo.

"Nina ishi na mama peke yake hivyo sina mtu wa kunihudumia viatu vya shule, madaftari, vitabu, sare za shule na mahitaji mengine ndiyo maana nakaba watu ili nipate mahitaji hayo" amesema Mohamed ambaye hadi sasa bado anasoma katika shule ya sekondari Itega kidato cha tatu.

Wengine wanaounda kundi hilo la Kamchape lililopo Kizota ni Abdul Mchangala (18), Mashaka Idd (17), Salum Mohamed (24) na Hamis Kikweli (40).

Kamanda Muroto ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu katika mkoa wa Dodoma pamoja na wale wanaonunua vitu kutoka kwa wahalifu kuwa adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527