TCRA YAWAKALIA KOONI MULTICHOICE (DSTV) NA ZUKU KWA KUTOONYESHA TELEVISHENI ZA NDANI

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) inakusudia kusitisha leseni ya kampuni ya Multichoice Tanzania Limited, wamiliki wa king’amzi cha DSTV na Simbanet Tanzania Limited inayomiliki Zuku kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukiuka masharti ya leseni.


Taarifa iliyowekwa kwenye vyombo vya habari na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, leo Agosti 7 inaeleza kuwa kampuni hizo zimejumuisha katika vifurushi vyao chaneli za ndani ambazo hazitakiwi kulipiwa.


“Simbanet Tanzania Limited, Multichoice Tanzania Limited, hairuhusiwi kuonyesha chaneli za televisheni zenye leseni za kutazamwa bila malipo kupitia ving’amuzi vyao isipokuwa TBC1 peke yake,” limeeleza tangazo hilo.


Tangazo hizo linasema TCRA imewahi kuziamuru kampuni hizo kuacha kubeba na kuonyesha chaneli hizo kwa kuwa ni kinyume na matakwa ya sheria na leseni walizopewa lakini zimekaidi onyo hilo na kuendelea kuonyesha chaneli hizo.


Limeongeza kuwa TCRA inakusudia kusimamisha kabisa leseni zote zilizotolewa na mamlaka hiyo kwa kampuni hizo kwa sababu zimeshindwa kutekeleza amri halali na masharti ya leseni zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527