MKUU WA MKOA AAGIZA WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWE MARA MOJA

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuanza msako wa kuwakamata wahamiaji haramu waliojificha kwenye mashamba na majumbani.

Alitoa agizo hilo jana Jumatatu Agosti 6, 2018 wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya ya Kasulu na Buhigwe ambapo alisema wahamiaji haramu mkoani humo wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wahukumiwe kifungo.

Katika hatua nyingine RC Maganga alioomba mahakama kuhakikisha kesi zote za wahamiaji haramu zinapewa kipaumbele ili kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani, ambao wanakula chakula bila kuzalisha.

Alisema kuna wahamiaji haramu na wakimbizi waliotoroka kambini wanaishi mitaani na kwenye nyumba za wananchi kinyume cha sheria, jambo ambalo halikubaliki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527