DC JOKATE ATOA MAAGIZO KWA WATAALAMU WA AFYA UNYONYESHAJI WATOTO

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto.

Amesema elimu hiyo itawawezesha kinamama kupata kizazi chenye afya bora na kushiriki vyema masuala ya uchumi na kijamii kwa siku zijazo.

Ameyasema hayo leo Agosti 7 muda mfupi mara baada ya kufunga maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji watoto duniani yaliyofanyika mjini humo kwa ngazi ya wilaya ya Kisarawe.

Hii ni kazi ya kwanza kwa Jokate tangu ateuliwe na kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

"Uongozi wa Serikali kwa ngazi zote mnapaswa kuweka misingi imara na kuhamasisha jamii yetu ili itilie maanani kunyonyesha watoto kikamilifu."

Jokate amewakumbusha waajiri kuzingatia sheria za ajira zinazowataka kuwapa likizo ya uzazi ya siku 84 ili waweze kunyonyesha watoto wao kikamilifu.

"Hii si kwa upande wa kinamama pekee bali hata kinababa nao wanapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku tatu pindi wake zao wanapojifungua na hizo siku wanapaswa wazitumie kuwapa misaada mbalimbali wake zao ili waweze kunyonyesha watoto wao kikamilifu," alisema Jokate.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post