KESI TIDO MHANDO YAPIGWA KALENDA TENA

Kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando imepigwa kalenda tena hadi Agosti 27, 2018 ambapo mashahidi wa upande wa Mashitaka wataendelea kutoa ushahidi wao.


Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa leo Alhamisi Agosti 16, 2018 lakini wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameieleza mahakama kuwa hawana shahidi na akaomba kesi ipangiwe tarehe nyingine ili iendelee kusikilizwa.


Hata hivyo, Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Muhina amesema Hakimu Mkazi Mkuu, Huduma Shaidi anayeiendesha kesi hiyo anaumwa na kupanga tena tarehe hiyo.


Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.