EMMANUEL RAMAZANI SHADARI KUMRITHI RAIS JOSEPH KABILA CONGO

Joseph Kabila

Sasa ni rasmi kwamba rais Joseph kabila wa Congo hatawania tena urais na kwamba chama chake kimemchagua Emmanuel Ramazani Shadari kuwa mrithi wake na mgombea wa uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba.

Tayari bwana Ramazani amewasilisha stakhabadhi zake za kuwania urais kwa tume ya ya uchaguzi mchana wa leo saa chache kabla ya muda uliowekwa kukamilika.

Emmanuel Shadari mwenye umri wa miaka 57 ni mwandani wa karibu wa rais Joseph kabila. Alikuwa katibu wa kudumu wa chama tawala cha PPRD na mtu muhimu wa kampeni za rais Kabila .

Akiwa waziri wa maswala ya ndani bwana Shedari alijulikana kuwa mtu asiye na huruma .

Shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch limesema kuwa anahusika pakubwa na usakaji wa kutumia nguvu wa viongozi wa upinzani na wafuasi wao mbali na kukamatwa kwa wanaharakati.


Ni miongoni mwa maafisa wanane wakuu serikalini waliolengwa na vikwazo vya muungano wa Ulaya mwaka uliopita

Wanachama wa muungano unaojulikana kama Common Front for Congo (FCC) awali waliitwa kwenda kasri la rais nje ya mji wa Kinshasa jana Jumanne kwa kile kilitajwa kuwa "mkutano muhimu.

Baada ya mazungumzo hayo ya mapema jana, msemaji wa Kabila Lambert Mende, aliwaambia waanidishi wa habari kuwa mgombea atajulikana mapema asubuhi.

Wakati wa mkutano wa Jumanne kwenye shamba lake, Rais Kabila aliwahutubia wale waliofika bila ya kutaja hatma yake ya kisiaisa.

Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 alikataa kuandoka mwishoni mwa mwaka 2016 wakati mihula yake miwili ya kikatiba ilikamilika lakini bado amekataa kusema ikiwa atawania tena.Jean-Pierre Bemba amewalisha makaratasi ya kuwania baada ya kurejea Kinshasa wiki iliyopita kufutiaa kuondolewa mashtaka na ICC

Baadhi ya wapinzani wake wanashuku kuwa kabila atajaribu kubaki madarakani na kuwania kwa muhula wa tatu licha ya katiba kutoruhusu hilo.

Sintofahamu hiyo imechangia kuzuka misukosuko ya kisiasa na kusababisha maandamano ya kumpinga kabila ambayo yamesababisha umwagikaji wa damu.

Baadhi ya watu ambao huenda wakapendekezwa na Kabila ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo; Mkuu wa watumishi wa rais, Nehemie Mwilanya Wilondja; na rais wa bunge la taifa Aubin Minaku.

Nchi ya Jamhuri wa Demokrasia ya Congo yenye karibu watu milioni 80 haijakuwa na mabadiliko amani ya madaraka tangu ipate uhuru wake mwaka 1960.Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), naye aliwasilisha makaratasi yake siku ya Jumanne.

Kabila ambaye sasa na miaka 47 alichukua madaraka kutoka kwa baba yake Laurent-Desire Kabila, ambaye aliuawa na mlinzi wake. Muda wake uongozi umekumbwa na ufisadi, kutokuwepo usawa na ghasia.

Shirika la Transparency International liliiorodhesha DRC nambari 156 kati 176 nchi fisadi zaidi duniani mwaka 2016. Mikoa mingi inakumbwa na mizozo na mamilioni ya watu wamekimbia makwao wengine wakielekea nchini Uganda, Tanzania, Angola na Zambia.


Wagombea ambao tayari wametangaza kuwa watawania urais ni Jean-Pierre Bemba, 55, mbabe wa zamani wa vita na hasimu wake Kabila ambaye alirejea Kinshasa wiki iliyopita baada ya kuondolewa mashtaka ya uhalifu wa kivita na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya huko Hague.Mwishoni mwa wiki iliyopita mamlaka zilimzuia Moise Katumbi, 53, mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga kuwasilisha makaratasi yake ya kuwania urais.

Mgombea mwingine wa upinzani Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), naye aliwasilisha makaratasi yake siku ya Jumanne.

Mgombea mwingine ambaye alitangaza kuwani Jumanne ni Tryphon Kin-Kiey Mulumba aliyekuwa wakati mmoja msemaji wa Mobutu Sese Seko na ambaye alihudumu mara mbili kama waziri wa serikali ya Kabila ambaya ni mgombea huru.

Mwishoni mwa wiki iliyopita mamlaka zilimzuia Moise Katumbi, 53, mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga kuwasilisha makaratasi yake ya kuwania urais.

Katumbi amekuwa akiishi nchini Ubelgiji tangu Mei mwaka 2016 baada ya kutofautiana na Kabila.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527