GARI LA WAGONJWA 'AMBULANCE' LAUA MGONJWA


Mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Bugwe, iliyoko wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, Hollo Paliga (10), amefariki baada ya gari la wagonjwa iliyokuwa inamkimbiza hospitalini kupinduka. 


Alifariki papo hapo baada ya gari hilo lililokuwa likimpeleka kwenda hospitali ya rufani ya mkoani Mbeya kwa matibabu zaidi kupata ajali na kupinduka katika Kijiji cha Magamba.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda, alisema kifo hicho kilitokea juzi saa 2:30 usiku katika Kijiji cha Magamba, gari likiwa kwenye barabara ya kutoka Mpanda kuelekea mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Alisema gari hilo la kubebea wagonjwa aina ya Landcruiser lenye namba za usajili DFPA 3273 lilikuwa likitoka Mpanda kwenda Mbeya kwa lengo la kumsafirisha mtoto huyo ambaye alikuwa amepewe rufani ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufani ya Mbeya akitokea Hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Kamanda Nyanda alisema baada ya kusafari kilometa 10 kutoka Mpanda mjini na kufika katika Kijiji cha Magamba lilipinduka na dereva ambaye jina limehifadhiwa alikimbia na polisi wanaendelea na kumsaka.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliosababishwa alishindwe kukata kona na kusababisha kupinduka.
Chanzo- Nipashe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527