EMMERSON MNANGAGWA AAPISHWA KUWA RAIS WA ZIMBABWE

Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuwa Rais wa Zimbabwe siku moja baada ya mshindani wake mkuu Nelson Chamisa kutangaza kukataa matokeo ya uchaguzi.

Mapema Jumapili waangalizi wa uchaguzi kutoka Marekani walisema nchi hiyo imekosa utamaduni wa uvumilivu wa demokrasia.


Siku ya Ijumaa mahakama ya kikatiba ilikataa madai ya upinzani kuwa udanganyifu ulifanyika ikisema kuwa hakukuwa na ushahidi.

Uchaguzi huo wa mwezi Julai ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa miaka mingi Robert Mugabe aondolewa madarakani mwaka uliopita.
Siku mbili baada ya uchaguzi huo watu 6 waliuawa kwenye ghasia kati ya jeshi na wafuasi wa muungano wa upinzani MDC, unaodai kuwa kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa alikuwa ameibiwa ushindi wake.

Saa kadhaa kabla ya Mnanganwa kuapishwa taasisi ya kiamataifa ya Marekani inayohusika na masuala ya Demokrasia ilisema mfumo wa Zimababwe haukuruhusu vyama vya kisiasa kutendewa kwa njia iliyo sawa na watu hawakuruhusiwa kupiga kura kwa njia huru.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527