BOSI WA TWAWEZA ANYANG'ANYWA HATI YA KUSAFIRIA NA UHAMIAJI

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, amesema Idara ya Uhamiaji inashikilia hati yake ya kusafiria tangu Julai 24, ambapo pia licha ya kuwa na hati ya dharura, juzi Agosti Mosi mwaka huu alizuiliwa kusafiri kwenda jijini Nairobi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Agosti 3, Eyakuze amesema aliitwa uhamiaji na kutakiwa kupeleka hati yake ya kusafiria bila kuwa na taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hilo.


“Niliitwa Uhamiaji nikahojiwa kidogo na kuambiwa nipeleke pasipoti yangu sikuona haja ya kukataa sababu ni haki yao kuchukua, ila hadi sasa sijapata tamko rasmi kwa nini wamechukua,” amesema.


Aidha, Mkurugenzi huyo amesema Twaweza wataendele kufanya kazi zao kama kawaida pamoja na changamoto wanazopitia, ikiwamo kutumiwa barua mbili na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ikiwahoji kuhusu uhalali wa programu yao Sauti za Wananchi na kuwataka wafafanue kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.