Picha : SAVE THE CHILDREN,KIWOHEDE WAENDESHA BONANZA KUPINGA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WATOTO USHETU, AFISA WA EU ASHUHUDIA

Shirika la Save The Children kwa kushirikiana na shirika la KIWOHEDE limeendesha Bonanza la Michezo katika kata ya Uyogo halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

Bonanza hilo  limefanyika Alhamis Agosti 30,2018 katika Viwanja vya shule ya Msingi Bukwimba katika kijiji cha Uyogo kata ya Uyogo na  kuhudhuriwa pia na Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers ambaye ametembelea mkoa wa Shinyanga kujionea maendeleo ya mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi unaochangia ndoa na mimba za utotoni.

Bonanza hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za unaotekelezwa na Shirika la Save The Children kwa kushirikiana na shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya -EU.

Miongoni mwa michezo iliyofanyika ni maigizo,nyimbo za asili,kucheza muziki na mpira wa miguu kati ya Wananchi ‘Uyogo Stars’ na Uyogo Sekondari ambapo mshindi ambao ni Uyogo Sekondari waliondoka na zawadi ya mbuzi baada ya kuichapa Uyogo Stars bao 2-1.

Pamoja na michezo hiyo pia kulifanyika mdahalo uliohusisha maswali na majibu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na mila na desturi ambapo wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba,shule ya Sekondari Uyogo pamoja na wananchi wa kata ya Uyogo walijadili madhara ya mila na desturi kandamizi ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.

Awali kabla ya bonanza, Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers alitembelea Kituo cha huduma na msaada kwa watu waliofanyiwa ukatili (Kituo cha huduma shufa ‘One Stop Center’) kilichopo katika Hospitali ya Mji Kahama pamoja na kutembelea ofisi za shirika la KIWOHEDE na halmashauri ya Ushetu.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Meneja wa Shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga Benety Malima akimtambulisha Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers (kulia) na Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes (kushoto) wakati wa bonanza la michezo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu mila na desturi kandamizi lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bukwimba katika kata ya Uyogo halmashauri ya Ushetu -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kulia ni Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers akinyoosha mkono kuwasalimia wananchi wa kata ya Uyogo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba wakishindana kucheza muziki wakati wa bonanza hilo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba wakiangalia burudani ya muziki kutoka kwa wanafunzi wenzao.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba akiwa ameshikilia vitabu vinavyohusu haki za watoto baada ya kuibuka mshindi wa kucheza muziki na kujibu maswali kwa ufasaha kuhusu ukatili wa kijinsia na kupatiwa zawadi ya vitabu.
Afisa Miradi wa Shirika la KIWOHEDE kutoka makao makuu Dar es salaam, Emmanuel Yohana akimuuliza swali mwanafunzi kuhusu haki za watoto.
Afisa Mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni kutoka shirika la KIWOHEDE, Victor Reveta akielezea kuhusu mradi huo unaotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Msanii wa nyimbo za asili Top Manyota akiimba wimbo kuhusu madhara ya mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa ndoa na mimba za utotoni na kusababisha watoto wakose haki zao ikiwemo ya elimu.
Kulia ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akifuatiwa na Meneja wa Shirika la Save the Children mkoa wa Shinyanga Benety Malima, Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers na Afisa Mtendaji wa kata ya Uyogo Edson Monela wakisikiliza kwa makini wimbo kutoka kwa msanii Top Manyota.
Msanii wa nyimbo za asili Top Manyota akionesha mbwembwe zake wakati akitoa elimu kwa njia ya wimbo juu ya madhara ya mila na desturi kandamizi katika jamii.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Katikati ni Mratibu wa Elimu ya afya ya uzazi,ujinsia na haki kwa vijana halmashauri ya Mji Kahama kata ya Zongomela, Amos Juma akiendesha mdahalo kujadili madhara ya mila na desturi kandamizi kwa watoto. Mdahalo huo ulihusisha wanafunzi na wananchi wa kata ya Uyogo.
Mratibu wa Elimu ya afya ya uzazi,ujinsia na haki kwa vijana halmashauri ya Mji Kahama kata ya Zongomela, Amos Juma akiuliza maswali kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Uyogo.
Mkazi wa kijiji cha Uyogo Julieth Elias akichangia mada wakati wa mdahalo kuhusu madhara ya mila na desturi kandamizi katika jamii.
Wananchi na wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba wakifuatilia mdahalo huo.
Mratibu wa Elimu ya afya ya uzazi,ujinsia na haki kwa vijana halmashauri ya Mji Kahama kata ya Zongomela, Amos Juma akitoa zawadi ya vitabu vinavyohusu haki za watoto kwa wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba walioshiriki mdahalo na kujibu kwa ufasaha maswali kuhusu mila na desturi kandamizi.
Mdahalo ukiendelea.
Kikundi cha Upendo kikitoa elimu ya madhara ya mila na desturi kandamizi kwa njia ya mchezo wa igizo.
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers,wafanyakazi wa shirika la Save The Children,KIWOHEDE,viongozi wa kijiji na kata ya Uyogo na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba na shule ya sekondari Uyogo wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja kwa pozi mbalimbali.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Bukwimba akipewa kitabu cha haki za watoto wakati wa zoezi la kugawa vitabu hivyo kwa washiriki wa bonanza hilo.
Mwanafunzi akipokea kitabu cha haki za watoto.
Mchezo wa mpira wa miguu ukawadia: Wachezaji kikosi cha timu ya Uyogo sekondari wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Uyogo Stars inayoundwa na wananchi wa kata ya Uyogo.
Wachezaji wa Uyogo Stars wakiwa katika picha ya pamoja.
Mchezaji wa Uyogo sekondari akiwa na mpira.
Hatari mpira wa kona katika lango la Uyogo Stars.
Wanafunzi na wananzengo wakifuatilia mpambano kati ya Uyogo Stars na Uyogo sekondari.
Mchezaji wa Uyogo Stars akiwa na mpira.
Wananchi wa Uyogo wakishuhudia mechi kati ya Uyogo Stars na Uyogo Sekondari.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Uyogo wakishangilia uwanjani baada ya timu yao kuibamiza Uyogo Stars bao 2-1.
Afisa Miradi wa Shirika la KIWOHEDE kutoka makao makuu Dar es salaam, Emmanuel Yohana akizungumza baada ya mechi kati ya Uyogo Stars na Uyogo Sekondari kumalizika.
Afisa Mtendaji wa kata ya Uyogo Edson Monela akikabidhi kifuta jasho cha shilingi 15,000/- kwa wachezaji wa timu ya Uyogo Stars waliofungwa magoli mawili kwa moja na Uyogo sekondari.
Afisa Mtendaji wa kata ya Uyogo Edson Monela akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi wa mchezo wa mpira wa miguu 'Uyogo Sekondari'. Kulia kwake ni Mdhibiti Ubora kutoka shirika la Save The Children,Kanuty Munisi,kulia ni Afisa Miradi wa Shirika la KIWOHEDE kutoka makao makuu Dar es salaam, Emmanuel Yohana.
Afisa Mtendaji wa kata ya Uyogo Edson Monela akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya mbuzi kwa kapteni wa timu ya Uyogo sekondari Pasian Benedicto.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Uyogo wakiwa wammbeba mbuzi wao ikiwa ni zawadi ya ushindi baada ya kuichapa Uyogo Stars bao 2-1.
Furaha ya zawadi ya mbuzi ikiendelea.
Wanafunzi wakiendelea kufurahia zawadi ya mbuzi.
Awali kabla ya bonanza: Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers (wa kwanza kulia) akiwa katika ofisi za shirika la KIWOHEDE mjini Kahama. Wa pili kushoto ni Afisa Miradi wa Shirika la KIWOHEDE kutoka makao makuu Dar es salaam, Emmanuel Yohana akielezea jinsi shirika hilo linavyoshirikiana na shirika la Save The Children kutekeleza mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi kwa watoto na wanawake katika wilaya ya Kahama.
Hapa ni katika Kituo cha huduma shufa ‘One Stop Center’ kilichopo katika Hospitali ya Mji Kahama ambapo Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers alitembelea ili kujionea namna kituo hicho kinavyotoa huduma kwa watu waliofanyiwa ukatili hususani watoto na wanawake. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Mji Kahama, Franaeli Reuben akielezea jinsi wanavyoshirikiana na shirika la Save The Children katika kuwahudumia watu waliofanyiwa ukatili.
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers akiipongeza serikali na shirika la Save The Children kuanzisha Kituo cha huduma na msaada kwa watu waliofanyiwa ukatili (Kituo cha huduma shufa ‘One Stop Center’) kilichopo katika Hospitali ya Mji Kahama na kuomba vituo vingi zaidi vianzishwe hata kwenye maeneo ya pembezoni ili wananchi wapate huduma.
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes nje ya Kituo cha huduma shufa ‘One Stop Center’) kilichopo katika Hospitali ya Mji Kahama.
Hapa ni katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu: Kushoto ni Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo,Christina Akyoo akimkaribisha Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers na viongozi wa shirika la Save The Children na KIWOHEDE.
Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo,Christina Akyoo akiushukuru Umoja wa Ulaya - EUkufadhili mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi kwa watoto na wanawake katika halmashauri hiyo unaotekelezwa na shirika la Save The Chidren kwa kushirikiana na KIWOHEDE.
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villiers akiishukuru halmashauri ya wilaya ya Ushetu kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya na Save The Children inayoshirikiana na KIWOHEDE katika kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa ndoa na mimba za utotoni.
Kulia ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akisisitiza jambo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527