BENKI YA NMB TAWI LA SHINYANGA YAENDESHA WARSHA WARSHA KWA WAFANYA BIASHARA 'NMB BUSINESS CLUB'

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Shinyanga Baraka Ladislaus  akionesha moja ya vyeti vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa wateja waliofanya vizuri kuchukua na kurejesha mikopo pamoja na matumizi sahihi ya kifedha.
 ***
Benki ya NMB tawi la Shinyanga imeendesha warsha ya mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo ,wa kati na wakubwa (NMB Business Club) mkoa wa Shinyanga kutambua fursa mbalimbali za kibiashara ili waweze kukuza mitaji na biashara zao.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Agosti 17,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga.

Akizungumza na wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa benki ya NMB tawi la Shinyanga Baraka Ladislaus alisema warsha hiyo ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na benki hiyo kwa wateja wake.

“Utamaduni huu wa mafunzo umeanza tangu mwaka 2009 ambapo unawakutanisha wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa ili kuwapa nafasi ya kutambuana, kujadili changamoto mbalimbali za masoko,lakini pia kupatiwa mafunzo ya elimu ya kibiashara”,alisema Ladislaus.

Meneja huyo alisema kutokana na changamoto ya elimu ya kibiashara ,Benki ya NMB imekuwa ikitoa fursa ya kuleta wakufunzi wa masuala ya kifedha watakaotoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na namna ya uendeshaji na unufaikaji katika biashara zao.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki ambao ni wafanyabiashara na wateja wa Benki ya NMB wameipongeza benki hiyo kwa hatua ya utoaji mafunzo ya kifedha pamoja na huduma rafiki.


Katika warsha hiyo Benki ya NMB imetoa vyeti kwa wateja waliofanya vizuri kuchukua na kurejesha mikopo pamoja na matumizi sahihi ya kifedha ili kuwavutia na kuwapa hamasa wateja kuendelea kutumia na kufurahia huduma hizo.

Na Malaki Philipo - Malunde1 blog

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO

Meneja wa Benki ya NMB tawi la Shinyanga Baraka Ladislaus  akitoa maelezo na kuonesha vyeti vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa wateja waliofanya vizuri kuchukua na kurejesha mikopo pamoja na matumizi sahihi ya kifedha
Wafanyabiashara wadogo ,wa kati na wakubwa (NMB Business Club) mkoa wa Shinyanga wakifuatilia matukio wakati wa warsha hiyo
Mteja wa Benki ya NMB  akipokea cheti ikiwa ni miongoni mwa wateja waliofanya vizuri kuchukua na kurejesha mikopo pamoja na matumizi sahihi ya kifedha
Mteja wa Benki ya NMB akionesha cheti
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea

Meza kuu wakinyoosha mikono ishara ya kuunga mkono huduma zinazotolewa na Benki ya NMB
Wafanyabiashara wakinyoosha mikono kuunga mkono huduma zinazotolewa na Benki ya NMB
Mteja wa Benki ya NMB akichangia hoja wakati wa warsha hiyo
Mteja wa Benki ya NMB akichangia hoja wakati wa warsha hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527