BASATA YAWATOA HOFU WASANII KUFUNGIWA KAZI ZAO


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza amefunguka na kuwataka wasanii wa muziki nchini, kufuta fikra zao walizojijengea vichwani mwao kuwa Baraza hilo lipo kwa ajili ya kufungia kazi zao tu.

Mngereza ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuwepo uvumi kwenye mitandao ya kijamii kwamba endapo msanii ataonekana kwenye ofisi za BASATA basi atakuwa ameitwa kwa ajili ya kuadhibiwa.

"Sio kila msanii atakayekuwa anaitwa BASATA basi anataka kufungiwa kazi zake, hiyo ni dhana tu ambayo imejengeka kwa baadhi ya watu. BASATA ipo kwa ajili ya kuwasaidia wasanii katika masuala mengi tu, maana hata mikataba yao pia tunashughulikia", amesema Mngereza.

Mbali na hilo, Mngereza amefafanua baadhi ya masuala kuwa, wapo wasanii wengine wamekuwa na utamaduni wa kwenda BASATA wenyewe kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali.
Chanzo-EATV
Theme images by rion819. Powered by Blogger.