BABU AFUNGA SMARTPHONE 11 KWENYE BAISKELI ILI ACHEZE ‘GAME’


Babu, Chen San Yuan, wa Taiwan, amefunga simu 11 kwenye baiskeli yake ili kila aendapo aweze kucheza michezo ya Pokemon iliyoko kwenye simu hizo.

Yuan, mwenye umri wa miaka 69 na anayeishi jiji la New Taipei, huzunguka na simu hizo kila mahali aendapo na akiingia mahali huzifungua kwenye baiskeli na kwenda nazo ili aweze kucheza wakati wowote.
Hulka hiyo ilianza mwaka 2016 wakati mjukuu wake alipomfundisha kucheza michezo hiyo ambayo imemjengea tabia hiyo ya kuutumia muda wake asipokuwa kazini kucheza michezo hiyo.
Licha ya kwamba simu hizo zimemgharimu Paundi 1,165 (Sh. mil. 3.3), bado anataka kununua simu nyingine zaidi ili zifike 15.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.