
Hatimaye mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani maarufu kama Mzee King Majuto umehifadhiwa nyumbani kwake huko Donge, Tanga nchini Tanzania.
Kabla ya kuhifadhiwa mwili huo ulisafirishwa jana usiku hadi Tanga ambapo ulisimamishwa njiani kuwapa mashabiki fursaya kutoa heshima zao za mwisho.
Dua ya kuaga mwili wa marehemu huyo aliyefariki Jumatano usiku akitibiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ilifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam





Social Plugin