ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA KOFFI ANNAN AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 18, 2018

ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA KOFFI ANNAN AFARIKI DUNIA

  Malunde       Saturday, August 18, 2018

Kofi Annan

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Kofi Annan amefariki dunia leo nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Katibu huyo mkuu wa zamani wa UN ndiye kiongozi wa mwafrika kushika wadhifa wa juu zaidi wa kidiplomasia duniani, alihudumu miaka 10 katika nafasi hiyo na kutunukiwa tuzo ya Nobel mwaka 2001 kutokana Kushughulikia haki za kibinadamu.

Aidha Annan alihudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kutafuta Amani na suluhu8 ya kudumu katika kutatua mgogoro unaendelea nchini Syria.

Historia ya maisha yake

Kofi Annan alizaliwa, 8 April, 1938 katika mji wa Kumasi nchini Ghana na kusoma elimu yake katika vyuo mbalimbali kikiwemo chuo cha sayansi na teknolojia cha mjini Kumasi ambacho sasa kinajulikana kama chuo cha sayansi na teknolojia cha Kwame Nkurumah, mwaka 1958 .

Alijiunga na Umoja wa Mataifa mwaka 1962, ambapo alifanya kazi katika shirika la afya duniani (WHO) na baadaye kuhamia katika shirika la wakimbizi duniani (UNHCR) . Mwishoni mwa miaka ya 1980, Annan aliteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika nafasi tatu mfululizo, rasilimali watu, ulinzi na usalama pamoja na mipango ya bajeti na masuala ya fedha.

Mwaka 1996, Kofi Annan alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN kuchukua nafasi ya Boutros Boutros-Ghali ambaye alisimamishwa katika uchaguzi huo licha ya kushinda kwa kura 14 kati ya 15 za baraza la usalama la UN.

Alistaafu nafasi ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2006 na baadaye mwaka 2007 alianzisha shirika lake lililojulikana kama ‘ Kofi Annan Foundation’ lililojikita katika utawala bora na kuimarisha amani ya nchi mbalimbali na dunia kwa ujumla.

Ameacha watoto wawili, Ama ambaye ni wa kike na mtoto wa kiume, Kojo ambao wote alizaa na mkewe raia wa Nigeria, Titi Alakija kabla ya kutengana mwaka 1983.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post