YANGA YAPATA MRITHI WA MKWASA


Pichani aliyekuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa (kulia), na Omary Kaaya.

Tetesi zinasema kuwa klabu ya Yanga imeanza kuziba mapengo ya watendaji wake kwa kumteua Omary Kaaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa.

Awali Kaaya alikuwa ofisa masoko wa klabu hiyo kabla ya Bodi ya wadhamini na kamati tendaji kumteua kukaimu nafasi ya Mkwasa.

Taarifa zinadai kuwa kikao cha dharura kilichofanyika jana baada ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga kutangaza kujiuzuru jana mchana.

Ofisa habari wa klabu hiyo Dismas Ten alipotafutwa kuzungumzia suala hilo simu yake iliita bila majibu na baadaye kuzima kabisa.

Julai 18, 2018 aliyekuwa Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa alitangaza kujiuzuru nyadhifa zake ndani ya wanajangwani huku sababu kubwa akieleza ndani ya barua yake kuwa ni matatizo ya kiafya.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.