Friday, July 6, 2018

WAWINDAJI HARAMU 'MAJANGILI' WAFARIKI KWA KULIWA NA SIMBA

  Malunde       Friday, July 6, 2018

Pichani ni Simba wakiwa mbugani

Majangili wawili wamefariki kwa kuliwa na Simba katika moja ya mbuga ya wanyama nchini Afrika Kusini walipokuwa wakitekeleza uwindaji haramu.

Askari wa doria nchini Afrika Kusini wamethibitsha kutokea kwa tukio hilo na kwamba waligundua mabaki yanayodhaniwa kuwa ya watu wawili mpaka watatu katika mbuga ya wanyama ya Sibuya iliyopo karibu na Kusini-Mashariki mwa mji wa Kenton.

Katika miaka ya hivi karibuni, Ujangili umeongezeka sana Afrika ya Kusini, na hii imetokana na kuongezeka kwa hitaji la pembe za Vifaru huko bara la Asia hasa China na Vietnam ambapo pembe za Vifaru zinaaminika kwa kuongeza hisia za kimapenzi.

Mmiliki wa hifadhi ya Sibuya, Nick Fox, akiongea na moja ya chombo cha habari amesema kuwa ilisadikika jumapili kuna watu wawili waliingia katika mbuga na jumanne askari wa doria walikuta mabaki ya miili hiyo.

Polisi wamesema kuwa Afrika Kusini imepoteza vifaru 7000 kwa muongo uliopita na kuongeza kuwa wanaendelea na msako ili kuangalia kama kuna majangili walionusurika.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post