VYAMA VYA SIASA VYAKUMBUSHWA KUZINGATIA SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI

Wakati tukielekea kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kata 77 utakaofanyika tarehe 12 Agosti, 2018, nachukue fursa hii kuwakumbusha wadau wote hususani vyama vya siasa, wagombea na Asasi za kiraia kuzingatia matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Sheria ya Gharama za uchaguzi inamtaka kila Mgombea wa Ubunge na Udiwani kuweka wazi mapato na matumizi ya gharama anazotarajia kuzitumia wakati wa uchaguzi husika kwa kujaza fomu maalumu ( EE1 & EE2) ambazo hujazwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka husika ndani ya siku saba, kuanzia siku ya uteuzi wa wagombea. Hivyo ninasisitiza ujazaji sahihi wa fomu hizo maalumu ili kukidhi matakwa ya Sheria.

Pia, ninawakumbusha wagombea, vyama vya siasa na umma kwa ujumla kuepuka kufanya vitendo vinavyokatazwa na Sheria za nchi hususani Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki na pia unaendeshwa katika hali ya Amani na utulivu.

Nichukue nafasi hii pia kuwatakia Wadau wote maandalizi na uchaguzi Mwema.

Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527