Thursday, July 5, 2018

MAAFISA WA USALAMA WATUHUMIWA KUTESA NA KUBAKA WANANCHI

  Malunde       Thursday, July 5, 2018

Wanajeshi wa Ethiopia katika doria

Ripoti mpya imechapisha jinsi maafisa wa usalama wa Ethiopia walivyowatesa na kuwabaka wafungwa wa kisiasa katika Jimbo la Somalia.

Ripoti hiyo iliyochapishwa na shirika la Human Rights Watch limewashutumu maafisa wanaofanya kazi katika Jela la Ogaden, pamoja na maafisa wa kikosi cha Polisi cha Liyu. Wengi wa wafungwa walioteswa walihusishwa na kundi la upinzani la Ogaden Liberation front lililopigwa marufuku.

Shirika la Human Rights Watch liliwahoji Zaidi ya watu mia moja, wengi wao waliokuwa wafungwa katika jela la Ogaden kati ya miaka ya 2011 na 2018.

Waathiriwa walikariri jinsi walivyovuliwa nguo zote kabla ya kupigwa mbele ya wafungwa wenzao.

Mmoja alisema kuwa alitengwa kifungoni kwa muda wa miaka mitatu, na aliondolewa kwenye seli nyakati za usiku tu ili ateswe.

Maafisa wakuu wa polisi na pia wa jela wameshutumiwa sio tu kwa kutoa amri kwa wafunga kuteswa na kubakwa, lakini pia kwa kushiriki matendo hayo.

Ripoti hiyo inasema kuwa watoto wengi wamezaliwa katika jela ya Ogaden, wengine wao wakidaiwa kupatikana kwa njia ya ubakaji uliotekelezwa na walinzi wa magereza.Waziri mkuu wa Ethiopia

Wafungwa wa kike wamesimulia jinsi walizaa wakiwa ndani ya seli, mara nyingi bila huduma za kiafya.

Wengi wa walioukuwa wafungwa wamesema hawajawahi kukabiliwa na shtaka la aina yoyote mahakamani.

Shirika la Human Rights watch linasema kuwa utesaji ni tatizo lililokithiri Ethiopia , na kuwa linapokea ripoti za watu kuhojiwa kikatili kutoka pembe zote za nchi mara kwa mara.

Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed, amekiri kuwa maafisa wa usalama wamewatesa raia, na sasa shinikizo zinaendelea kuongezeka kwa wale wanaofanya matendo haya kuwajibika.
Chanzo- BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post