Thursday, July 5, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUFANYA ZIARA YA SIKU TANO SHINYANGA

  Malunde       Thursday, July 5, 2018


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Shinyanga itakayoanza Juali 7,2018 hadi Julai 11,2018 - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
***
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa atafanya ziara ya kikazi mkoani Shinyanga katika halmashauri zote sita za wilaya kuanzia Julai 7,2018 hadi Julai 11,2018.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Julai 5,2018,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amesema lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za maendeleo,kukagua masoko ya pamba pamoja na kuzungumza na wananchi na watumishi wa umma kwa kila halmashauri.


"Tutampokea Mheshimiwa Waziri Mkuu,Julai 7,2018 katika manispaa ya Shinyanga ambapo ziara yake itaanza kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa,Julai 8 atakuwa katika halmashauri ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga na baada ya hapo ataendelea na ziara katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kisha Kahama Mji,Ushetu na kumalizia ziara Msalala Julai 11,2018",alieleza Telack.


"Tarehe 10 Julai,2018 Mheshimiwa Waziri Mkuu atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mpango wa Bima ya Afya kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika ambao kitaifa utafanyika katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu wilayani Kahama",aliongeza Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Shinyanga itakayoanza Juali 7,2018 hadi Julai 11,2018 - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post