Thursday, July 5, 2018

MUNA LOVE AMTAJA BABA HALALI WA PATRICK

  Malunde       Thursday, July 5, 2018
Ni siku mbili zimepita toka taarifa za kifo cha mtoto wa Muna Love anayejulikana kwa jina la Patrick afariki dunia akiwa Nairobi nchini Kenya akipatiwa matibabu ambaye alifariki July 3,2018.

Baade taarifa zilienea kuhusiana na Peter Zacharia Komu aliyejitokeza na kudai ni baba mzazi wa Marehemu Patrick na kutaka msiba ufanyike nyumbani kwakwe Mwananyamala huku taarifa nyingine zikidai baba wa mtoto ni mtangazaji wa Clouds Tv Casto Dickson.

Kupitia instagram account ya Munalove amefunguka kuhusiana na mvutano ambao umekuwa ukiendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na baba mzazi wa marehemu Patrick.

“Jaman jamani 😭😭😭😭😭😭 naomba nimzike mtoto wangu 😭😭😭😭 vaeni viatu vyangu. Kuna siri kumbwa amjawahi kuijua nawaomba nimzike mtoto wangu alafu ndiyo mnitukane. Mimi 😭😭😭😭😭😭 naumia jamani, namuheshimu Peter siwezi kuweka kitu hapa maana nitamwaibisha….

"Siwezi kumsema Casto maana yeye anajua wapi alikosea, nawaombeni jamani, naomba nataka kumzika mwanangu. Miaka miwili nahangaika na Paty wangu 😭😭😭😭😭😭😭😭, nimalize kumzika niongee.

"Nyie wanawake mnaonihumuku, vaeni viatu vya siri nilizohifadhi… baba wa mtoto ni Casto, inatosha 😭😭😭😭😭😭😭😭, nitukaneni mimi nife ila Paty ni kiongozi alieniongoza nione maisha mapya na nimjue Mungu… Nitalia milele mimi.

"Paty wangu😭😭😭😭😭😭😭😭leo wanakugombania mwaanangu, natamani urudi mara moja😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭… Mwanangu ntaleta ijumaa na ntamzika Jumamosi😭😭😭😭😭, msiba uko kwangu Mbezi Beach.” amesema Muna. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post