SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA GAWIO LA BIL 717 | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 23, 2018

SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA GAWIO LA BIL 717

  Malunde       Monday, July 23, 2018

Serikali imepokea gawio la Sh717.56 bilioni kutoka kwa kampuni, taasisi na mashirika ya umma kwa ajili ya mwaka 2018.

Akizungumza katika hafla ya kupokea gawio hilo leo Julai 23, 2018 jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka amesema gawio hilo ni kutoka kwa kampuni, taasisi na mashirika ya umma 43 kati ya 90 ambayo yanastahili kutoa gawio.

Mbutuka amesema changamoto iliyopo ni kuwa kuna baadhi ya kampuni zisizozingatia ubia baina yao na Serikali. Amesema zipo ambazo hutangaza kutoa gawio kwa wanahisa lakini hushindwa kuwasilisha serikalini.

Msajili amesema viwanda vingi vimekuwa vikisuasua akieleza kati ya 51 vilivyofungwa 12 vilikiuka masharti ya mkataba na wawekezaji wake hawakuonyesha nia ya kuviendeleza.

Amesema Hazina imetoa ilani kwa wawekezaji tisa kuonyesha nia ya Serikali kuvitwaa viwanda na kuviendeleza.

“Ubinafsishaji ulikuwa na nia ya kuongeza tija na isitafsiriwe kama tunafanya utaifishaji, tutavichukua, tutatangaza na kuwapa wawekezaji wengine ili kutimiza shabaha tuliyojiwekea,” amesema.

Amesema viwanda vitatu vimerejeshwa serikalini na wawekezaji wengine wamepewa.
Chanzo-Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post