SAED KUBENEA : SIONDOKI CHADEMA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 30, 2018

SAED KUBENEA : SIONDOKI CHADEMA

  Malunde       Monday, July 30, 2018
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema hana mpango wa kuhamia CCM kutokana na madhira aliyoyapata.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2018 Kubenea amesema hana sababu hata moja ya kuipenda CCM.

“Mimi siondoki humu kama kuna mambo ya kurekebisha ndani ya chama nitarekebisha nikiwa humu. Nikishindwa kurekebisha nitaacha na kufanya shughuli zangu kwa sababu mimi ni mwandishi wa habari, nitarudi kwenye kazi zangu."

Kubenea amefafanua kuwa wanaofanya mchezo huo mchafu wa kuchafuana ni vijana wa Chadema.

Kuhusu kushutumiwa na chama amesema kuna taratibu ikiwamo kuitwa kwenye kamati ya maadili kitu ambacho hajawahi kufanyiwa.

"Nashutumiwa vipi na sijawahi hata kuhojiwa na kamati yoyote,"

Amesema yeye ni mbunge kwa miaka mitano, hivyo atakuwa na Chadema kwa muda wote labda Mungu aichukue roho yake.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post