RAIS MAGUFULI AMLILIA PROFESA MAJI MAREFU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mkoani Tanga Steven Hillary Ngonyani maarufu “Profesa Majimarefu”.


Profesa Majimarefu amefariki dunia usiku Julai 2, 2018 katika katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.


Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na kifo cha Profesa Majimarefu ambaye alikuwa Mbunge hodari na aliyewapenda na kuwapigania wananchi wa Jimbo lake la Korogwe.


“Spika Ndugai nimehuzunishwa sana na kifo cha Profesa Majimarefu, tumempoteza mtu aliyejitoa kuwahudumia wananchi kwa juhudi zake zote, aliyependa maendeleo na aliyekuwa rafiki wa watu, nakupa pole sana wewe Spika, Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na wote walioguswa na kifo hiki”amesema Rais Magufuli.


Rais Magufulli amemuombea Profesa Majimarefu apumzishwe mahali pema peponi.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.