POLISI KUTUMIA MANATI BADALA YA BUNDUKI KUDHIBITI WAHALIFU


Gavana wa mji wa Veracruz nchini Mexico Miguel Angel amewataka Polisi katika mji wake kuanza kutumia manati kukabiliana na wahalifu badala ya kutumia bunduki.


Imeelezwa kuwa Gavana Miguel amechukua uamuzi huo baada ya Polisi 30 kati ya 130 kufaulu jaribio la kutumia bunduki na kudhihirisha kuwa Maafisa wengi wa Polisi hawajui kutumia bunduki vizuri kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa raia.

Imedaiwa kuwa miji mingine mathalani Ciudad Mendoza, Pueblo Viejo na Ixtaczoquitlan ya chini humo nayo imewakataza Polisi wake kutumia bunduki badala yake imewagawia Manati ili kukabiliana na wahalifu.

Aidha maamuzi hayo ya Gavana Miguel yamekosolewa sana na Meya wa mji huo kwa madai kwamba Polisi kutumia Manati kuwalinda Watu na mali zao ni kichekesho kwani hawatoweza kukabiliana na wahalifu wanaotumia silaha kali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527