OFISA WA POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI MOROGORO


Ofisa wa Jeshi la Polisi ambaye ni Mkufunzi katika Chuo cha Polisi Kidatu Morogoro, Benedict amejiua kwa kujipiga risasi leo alfajiri Julai 12, 2018 .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo RPC Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha amesema “Tukio limetokea Alfajiri leo, Ofisa amejipiga risasi kidevuni ikatokea kichwani, mwili wake umehifadhiwa unasubiri uchunguzi na Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kina kufahamu chanzo cha kujipiga risasi”.

Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi wote wanapokuwa na matatizo kuwashirikisha watu wengine ili liweze kutatuliwa kuliko kujiua.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.