Mashabiki wakisherehekea Zagreb
Mashabiki wa Croatia walisherehekea usiku kucha baada ya taifa lao kuwaondoa England kutoka kwa michuano ya Kombe la Dunia Urusi na kufuzu kwa fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa, England waliomboleza.
Croatia walipata ushindi wa 2-1 baada ya mechi kumalizika sare ya 1-1 muda wa ziada.
Mashabiki walijaza uwanja ulio katikati mwa mji mkuu wa Croatia wa Zagreb wakiimba na kupeperusha bendera za taifa hilo. Baadhi walijitumbukiza hadi kwenye chemchemi za maji zinazopamba uwanja huo.
Mabao yalivyofungwa
Kieran Trippier dakika ya 5 Croatia 0-1 England
Ivan Perisic dakika ya 68 Croatia 1-1 England
Mario Mandzukic dakika ya 109 Croatia 2-1 England
Croatia ni taifa la watu milioni nne hivi na ni moja ya mataifa yenye idadi ndogo sana ya watu kuwahi kufika fainali Kombe la Dunia.
Watakutana na Ufaransa katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Jumapili kwa fainali saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.
England watakutana na Ubelgiji mechi ya kuamua atakayemaliza nafasi ya tatu, mechi ambayo itachezewa mjini St Petersburg.
Kwa Croatia kukiwa kicheko na shangwe, kwa raia wa England kulienda masikitiko, huzuni na majonzi.
Mashabiki wakisherehekea Zagreb
Mashabiki wengi walijitokeza Zagreb
Mashabiki wakicheza kwenye maji kusherehekea katikati mwa mji wao mkuu Zagreb
Rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarovic (kushoto) alimpa waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jezi ya taifa hilo wakati wa mkutano mkuu wa Nato mjini Brussels, Ubelgiji
Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric (kati) akiwa na Mario Mandzukic (kulia) wakisherehekea Luzhiniki, Moscow
Shabiki huyu kwa jina Daniel alisherehekea kwa kinywaji, na aliambia BBC kwamba "ushindi huo ni mkubwa mno" kwa taifa hilo ndogo
Hali ilivyokuwa kwa England:
Walianza kwa matumaini baada ya bao kufungwa dakika za kwanza lakini baadaye wakavunjwa moyo.

Ndoto kwisha: Mashabiki wakifarijiana katika bustani maarufu ya Hyde Park jijini London
Shabiki mdogo wa England akiliwazwa Castlefield Bowl, Manchester
Katika bustani ya Hyde Park, London, takriban mashabiki 30,000 walifika kutazama England wakicheza nusufainali, mkusanyiko mkubwa wa watu London kutazama mchezo wa kandanda tangu Euro 96.
Shabiki huyu labda alizidi katika kusherehekea kabla ya mechi Urusi
Shabiki wa England akisherehekea karibu na shabiki wa Croatia kabla ya mechi Urusi
Maelfu ya mashabiki Hyde Park kabla ya mechi kumalizika
Wakati wa muda wa ziada Hyde Park
Mashabiki wa England wakitokwa na machozi Manchester
Manchester wakisherehekea baada ya England kufunga bao la kwanza
Mashabiki wakitokwa na machozi Brighton Beach
Mashabiki waliovalia barakoa za Harry Brighton Beach
Shabiki wa England, Hyde Park
Mashabiki walivyokuwa wakisherehekea awali Nottingham Castle
Lily Harkin mwenye miaka minane alikuwa ameandika mgongoni mwa Cole Bryceland, Nottingham kwa matumaini, 'Kombe linarejea nyumbani', lakini baadaye 'England walirejea nyumbani' bila kombe
Roho mkononi Millennium Square, Leeds
Masikitiko Hyde Park
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin