Thursday, July 12, 2018

MWALIMU ANAYEDAIWA KUBAKA MWANAFUNZI WAKE AKAMATWA

  Malunde       Thursday, July 12, 2018
Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mwalimu wa shule ya sekondari Loliondo, Erick Kalaliche mkoani Lindi ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Loliondo kabla ya mwalimu huyo kuhamishwa.


Hayo yamebainishwa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'anzi baada ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha kutoa agizo la kutafutwa na kukamatwa kwa mwalimu huyo ambaye ametenda kosa la jinai na kuhamia katika shule nyingine.


"Agizo la Naibu Waziri wa Elimu tumelipokea na kama inavyofahamika kuwa kumpa ujauzito mwanafunzi ni kosa la jinai na jarada limeshafunguliwa la kupeleleza tukio hilo kwasababu baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wake yule
mwalimu alipewa uhamisho tangu mwaka 2017 lakini tumewasiliana na wenzetu katika kituo chake kipya kule Lindi na wametuambia kwamba wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo leo hivyo tunafanya mpango wa kurudishwa huku kwenye kesi yake", alisema Kamanda Ng'anzi.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu William Ole-Nasha amesisitiza kuwa, Wizara yake haiwezi kuvumilia walimu wanaofundisha watoto ambao pia ni kama wazazi wanaofumbia macho vitendo vichafu ambavyo vinarudisha nyuma sekta ya elimu na juhudi za serikali za kuhakikisha watoto wa kike wanapata haki yao ya elimu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post