Thursday, July 12, 2018

MWANAMKE AKATAA KUOLEWA NA MWANAUME ALIYEMPA FIGO

  Malunde       Thursday, July 12, 2018
Leo July 12, 2018 Mwanaume anayeitwa Simon Louis (49) amekataliwa ombi lake na mpenzi wake la kumuoa Mary Emmanuella (41) ambaye ni mpenzi wake aliyempenda mpaka kuokoa maisha yake mara baada ya kujitolea figo yake kumpandikizia na kunusuru maisha yake pindi figo zake zilipofeli.

Hata hivyo Simon alipohojiwa na Mwandishi wa Metro UK alisema kuwa hajutii maamuzi yake ya kumpa figo mwanamke huyo aliyempenda hata mara baada ya kukataa ombi lake alipopona ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

“Nilimpa moyo wangu, lakini pia nilijifikiria nikampa na figo yangu, chochote kilichotokea sijutii wala sitojutia kwa kumpa zawadi ya maisha,” amesema Simon.

Aidha Mary Emmanuella amesema ataendelea kuwa rafiki wa karibu wa Simon.

“Ni rafiki yangu sana na daima itakuwa hivyo, mapenzi kati yetu ni ya kweli, Simon angefariki kwa kile alichokifanya kwa ajili yangu,” amesema Simon
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post