Thursday, July 12, 2018

LUKA MODRIC : WAINGEREZA WALITUDHARAU SISI

  Malunde       Thursday, July 12, 2018
Moja kati stori zilizochukua headlines sana kwa sasa katika soka ni game ya nusu fainali ya pili kati ya England dhidi ya Croatia, kwani baada ya England kutolewa katika michuano hiyo kwa kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Croatia, kimewashangaza wengi kwani hawakutarajia.Mashabiki wengi wa England waliyokuwa Urusi na hata England walikuwa wameanza kushangilia kwa kauli yao ya “Its Coming Home” wakiashiria kuwa Kombe linakuja nyumbani, huku mashabiki wengine wakichora tattoo za kuonesha kuwa England Bingwa tayari.

Bahati mbaya mambo yamekuwa tofauti na England wametolewa kwa kufungwa goli 2-1, hivyo ndio mwisho wa ndoto yao baada ya game hiyo nahodha wa Croatia Luka Modricaliongea na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa England waliwachukulia poa.

“Waliidharau Croatia usiku wa leo na ndio lilikuwa kosa lao kubwa maneno yote hayo kutoka kwao tuliyasoma na kusikia na tukasema tutatona nani atachoka leo, hatukuchoka na tulimiliki mpira kiakili na kimwili kama nilivyosema awali walipaswa kuwa wapole na kuheshimu timu pinzani”>>> Luka Modric


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post