MGOMBEA UDIWANI MWINGINE WA CHADEMA AJIONDOA...KASEMA ' KAAMUA KUACHA TU' | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 31, 2018

MGOMBEA UDIWANI MWINGINE WA CHADEMA AJIONDOA...KASEMA ' KAAMUA KUACHA TU'

  Malunde       Tuesday, July 31, 2018
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara, Omari Kipanga, amekiri kupata nakala ya barua ya kujitoa kwa Mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Muungano, halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Mkurugenzi huyo amepokea barua hiyo ya mgombea udiwani  kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Ismail Liuye jana ikiwa ni siku chache zimesalia kabla ya kufikia uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

Taarifa zinaeleza kuwa Bw. Liuye amejitoa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kupokea vitisho kwa kutoka kwa watu mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi, akitishiwa maisha yake pamoja na familia yake.

Hata hivyo baada ya kuzungumza na bwana Liuye amedai kwamba ameamua kuacha kutokana na kwamba ni uamuzi wake.

"Mimi siendelei na kampeni, nimeacha. Nimeacha tu. Mtu unapoamua kuacha kitu si unaacha tu. Sababu nilizonazo ni za kwangu binafsi. Kama inasemekana kuhusu kutishiwa iendelee kusemekana".Amesema

Hata hivyo Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kwa sasa bado hana taarifa za kuhusu kujiondoa kwa mgombea wao katika kinyang'anyiro hicho na kwamba anachoamini kampeni zilikuwa zikiendelea labda awe amejiondoa baada ya Kampeni za jana  na kwamba bado anafuatilia habari hizo.

Pamoja na hayo Mkurugenzi Kipanga ameeleza kutokana na muda wa kuweka wagombea kupita, mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM, Hassan Likuto, atapita bila kupingwa kutokana na kutokuwapo kwa mgombea wa Chama kingine hivyo wanachosubiri ni taratibu za Tume waweze kumtangaza Likuto.

Hata hivyo amesema uchaguzi bado unaendelea katika Kata nyingine mbili zilizosalia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post