Breaking : MBUNGE MWINGINE WA CHADEMA AJIUZULU NA KUHAMIA CCM

Julius Kalanga aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chadema amejiuzulu nafasi zake zote ikiwemo Ubunge na kuhamia CCM usiku wa kuamkia leo.Katika sababu mojawapo ya kujiuzulu aliyoieleza,amesema ni Kuunga mkono juhudi kubwa za kuleta maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.

"Siwezi kuwa sehemu ya kukwamisha maendeleo ya wananchi wa Monduli kwa kupinga kila kitu. Ubunge si tatizo kwangu naweza kuwa mkulima au mfugaji ila si kuwa kikwazo," amesema Kalanga


Hapo pichani alikuwa akitambulishwa rasmi usiku na Msemaji wa chama cha CCM,Ndugu Pole.


Kufuatia uamuzi huo jimbo la Monduli liko wazi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.