Tuesday, July 10, 2018

MADIWANI WATATU WA CUF WAVULIWA UDIWANI TANGA

  Malunde       Tuesday, July 10, 2018
Chama cha Wananchi (CUF), jijini Tanga kimewavua uanachama madiwani watatu wakiwamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa Kata ya Mwanzange.


Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji, ametangaza hatua hiyo jana jioni baada ya kupokea barua kutoka kwa uongozi wa chama hicho.


“Nimepokea barua kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Taifa, Magdalena Sakaya ikeleza kuwafuta uanachama kwa madiwani wawili wa Viti Maalumu, Halima Juma na Fatuma Hamza na Diwani wa Kata ya Mwanzange, Rashid Jumbe,” amesema Mayeji.


Amezitaja sababu tatu zilizoainishwa katika barua hiyo kukivuruga chama, kukataa wito wa kamati ya maadili ya chama hicho na kukaidi kufika katika kikao cha Baraza la Uongozi Taifa la chama hicho.


Akizungumza baada ya uamuzi huo kutangazwa, Jumbe ambaye pia wa Mwenyekiti wa CUF wilaya, amesema hatambui waliomfuta uanachama kwa sababu si viongozi wala wanachama wa chama hicho.


Wakati huo huo, madiwani hao wa Viti Maalumu nao waliungana na Jumbe wakidai hawatambui uamuzi huo kwa sababu hawamtambui Sakaya wala Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba kwa sababu alishafukuzwa uanachama.


“Walioandika barua za kutufukuza sisi hatuwatambui, kiongozi tunayemtambua ni Katibu Mkuu wetu Maalim Seif Sharrif Hamad hao wengine hatuwajui,” wamesema.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post