LUGOLA AFUNGUKA GUMZO LA SUTI ZAKE ZENYE MIFUKO YA BENDERA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 21, 2018

LUGOLA AFUNGUKA GUMZO LA SUTI ZAKE ZENYE MIFUKO YA BENDERA

  Malunde       Saturday, July 21, 2018
Baada ya suti za Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali, mwenyewe amefunguka na kufafanua juu ya suala hilo.

Kwa muda sasa, tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, Lugola amekuwa akivaa suti zenye bendera ya Tanzania kwenye mifuko hali ambayo imesababisha mijadala kwenye mitandao ya kijamii.


Akizungumza na Michuzi, Lugola alisema anazo suti nyingi za aina hiyo na ni yeye mwenyewe aliyeamua zifanane kwa mwonekano.


Baadhi ya wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakihoji iweje Waziri avae suti moja muda mrefu wakidhani kuwa amekuwa akiirudia.


Lakini mwenyewe jana alijibu na kueleza kuwa suti hizo ambazo ameziita kuwa ni za aina yake, anazo nyingi lakini ameamua zote zifanane.


“Hata ninapobadilisha suti hizi hakuna anayeweza kujua kwa sababu zote zimefanana,” alisema.


Mwonekano wa suti hizo umefanya watu wengine kuzishangaa kutokana na mifuko ya shati kutengenezwa kwa bendera ya taifa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post