KANGI LUGOLA AKUTANA 'LIVE' NA IGP SIRRO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 21, 2018

KANGI LUGOLA AKUTANA 'LIVE' NA IGP SIRRO

  Malunde       Saturday, July 21, 2018
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola jana amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Sirro na Maofisa wengine Wakuu wa Jeshi hilo, Makao makuu ya Polisi Dar es salaam.


Waziri Lugola amekutana na IGP Sirro kukiwa na mfululizo wa maagizo aliyoyatoa ikiwemo kumtaka IGP Sirro amwambie kama wamewashindwa majambazi kutokana na kulazimika shughuli nyingi kufungwa inapofika jioni kwa kuhofia kuvamiwa.


Jambo la pili ilikuwa ni kutaka maelezo ya alipo Mbwa maalum wa Kikosi cha Bandari ambapo mpaka jana asubuhi ya July 20 2018 alikuwa hajapatikana. 

Baada ya Kikao hicho, Lugola alisema kilikuwa ni cha majumuisho ya zaiara zake ambapo ametoa mwezi mmoja zaidi kwa jeshi la polisi ili waandae ripoti kuhusiana na changamoto ya mbwa wa Bandarini pamoja na mpango mkakati wa kuwawezesha wananchi kufanya kazi zao usiku walau kwa baadhi ya maeneo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post