CHELSEA YATANGAZA KOCHA MPYA

Siku moja baada ya club ya Chelsea kutangaza kuwa wamemfuta kazi kocha wao Antonio Conte baada ya kudumu nae kwa miaka miwili akiwapa mataji ya EPL na Kombe la FA.
Leo club ya Chelsea imemtangaza rasmi kocha wa zamani wa Napoli Maurizio Sarrikuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu, Sarri anajiunga na Chelsea baada ya kuitumikia Napoli kwa miaka mitatu.
Sarri nafasi yake katika club ya Napoli ilitangazwa mapema kuchukuliwa na Carlo Ancelotti “Najisikia fahari kujiunga na Chelsea na kuja kufanya kazi premier League, najisikia fahari kuanza kazi na kukutana na wachezaji Jumatatu”, Maurizio Sarri
Theme images by rion819. Powered by Blogger.