KAULI YA "CCM ITATAWALA MILELE" YAWAPA PRESHA CHADEMA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 25, 2018

KAULI YA "CCM ITATAWALA MILELE" YAWAPA PRESHA CHADEMA

  Malunde       Wednesday, July 25, 2018
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kauli kuwa hadi ifikapo mwaka 2020 upinzani hautakuwepo na ile ya CCM itatawala milele, zinazidi kuwapatia mashaka.


Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa CHADEMA , Benson Kigaila amesema kauli hizo na yale yanayojiri katika uchaguzi mdogo, vinawapa shaka kuwa kuna mpango usio wa heri.


“Tumepata nyaraka inayosambaa kwenye mitandao ina nembo ya Tume (ya Taifa ya Uchaguzi) na CCM wanaitumia kujitapa kushinda kata 30. Tunashindwa kuelewa kwa nini hatujapewa vyama inazunguka mitandaoni,”


Akizungumzia juu ya namna wanavyodhulumiwa Kigaila amesema kwamba “Kata za Halmashauri ya Iringa Mjini pia wagombea wameondolewa kwa uonevu,”.


Hata hivyo kauli hii ya Bw. Kigaila inakuja ikiwa tangu siku moja ipite tangu Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri Jame kusema kwamba CCM imejiandaa kupima ‘mitambo’ yake katika uchaguzi huo mdogo ili kuhakikisha inakifuta CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.


Katika kampeni hizo, James alisema kwamba “Nataka kuwaambia kwa namna mitambo yetu ilivyofungwa hakuna mgombea wa upinzani ambaye atashinda, na mwaka 2020 CHADEMA watabaki labda ya majimbo mawili tu kusini moja na kaskazini moja,”


Alisema katika kuhakikisha kazi zinafanyika vizuri, wabunge wa upinzani wataporomoka wote mwaka 2020 na CCM itakaa yenyewe ili kupitisha mambo ya maendeleo kwa Watanzania.


Hata hivyo kauli Mwenyekiti wa UVCCM haijapishana na ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rais John Magufuli kwamba chama hicho kitatawala milele


“CCM ni chama tawala na kitaendelea kutawala milele na milele. Kwa wanaohangaika watapata tabu sana siku zote, siku hakuna mbadala ni CCM hadi milele. Wanachama wa CCM tembeeni kifua mbele tumeamua kuleta Tanzania mpya inayowapigania wananchi hasa wanyonge ili waweze kushiriki katika maendeleo,” alisema Dk. Magufuli.


Katika uchaguzi mdogo unaoendelea CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuchezewa rafu na wapinzani wao huku wakieleza kwamba dola, pamoja na Tume ya uchaguzi imekuwa ikiwapendelea wenzao.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post