KANGI LUGOLA AWAGEUKIA ZIMAMOTO


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametoa onyo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuacha mara moja tabia ya kutokwenda kwenye matukio ya moto kwa kisingizio cha kutokuwa na vifaa vya kutosha.

Akizungumza mapema leo alipowasili makao makuu ya Zimamoto jijini Arusha ambapo yupo katika ziara yake ya kikazi, Lugola ameagiza askari ambao hawataki kufanya kazi wasukumwe na kama hawataki na watachukuliwa hatua.

“Ole wenu niwasikie moto unawaka eti mmeshindwa kufika eneo la tukio kwasababu ya gari limeharibika, sawa gari limeharibika lakini nyie ni wazima mnaweza kwenda”, amesema Waziri Lugola.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Waziri huyo alipowashusha vyeo makamanda wawili kwakushindwa kudhibiti ajali, ambao ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya pamoja na Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Kagera ambapo alidai kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527