KANGI LUGOLA AVUNJA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI NA MABARAZA YOTE YA MKOA


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amelivunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na mabaraza yote ya ngazi ya mkoa.


Ametangaza uamuzi huo leo Julai 5, 2018 jijini Mbeya alipozungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mbeya na baraza la usalama barabarani mkoani humo.


Lugola amesema hajaridhishwa na utendaji wa baraza katika kukabiliana na ajali za barabarani.


"Nilikuwa namuuliza mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani nikabaini hajui hata sheria inayoliweka baraza hilo na hata kanuni zake hazijui, hii inaonyesha hatuna baraza na kuanzia sasa kwa mamlaka niliyonayo nalivunja baraza hili na nitaliunda upya," amesema Lugola.
Na Godfrey Kahango, Mwananchi 

Theme images by rion819. Powered by Blogger.