Friday, July 6, 2018

JINSI LUGOLA ALIVYOMTIMUA KWENYE KIKAO KAMISHNA WA MAGEREZA

  Malunde       Friday, July 6, 2018

 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukiza kikaoni, Kamishna wa Magereza, Juma Malewa kwa kosa la kuchelewa.Lugola amefanya hayo leo, Julai 6 wakati wa kikao cha kimkakati cha viongozi wa taasisi za wizara hiyo.


Lugola aliagiza mlango kufungwa saa 5 kamili wakati kikao hicho kinaanza. Lakini saa 5:1 Dk Malewa aliingia na hapo hapo Lugola alimwambia atoke nje.


"Nani anayefunguliwa mlango wakati nimesema saa 5 kamili asifunguliwe mtu kuingia kwenye kikao changu isipokuwa mwandishi wa habari?” amesema Lugola


Dk Malewa akajibu: “Ni Mimi hapa, samahani sana.”


Lugola: “hakuna cha samahani hapa.”


Dk Malewa: “Mheshimiwa nimeshafika hapa.”


Lugola: “Hapana hapana rudi nje, nikisema saa 5 ni saa 5 kwa hiyo am very sory (samahani sana).”


Akaongeza: "Wote mliochelewa naomba mtoke nje nawaheshimu sana, tena wengi ni maofisa wakubwa wa magereza lazima tuwe na jeshi lenye nidhamu. Naomba uende nje nakuheshimu sana.”


Hata hivyo baada ya kuzungumza na wanahabari Dk Malewa na maofisa wengine waliruhisiwa kuingia ndani ya kikoa hicho.


Na Bakari Kiango, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post