AZAM FC YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA WAKE MKUU HANS VAN DER PLUIJM


Kocha Hans van der Pluijm (kulia) wakati anatambulishwa na Azam FC leo.


Klabu ya Azam FC leo imemtambulisha rasmi kocha wake Mkuu Hans van der Pluijm, ambapo baada ya utambulisho ameweka wazi mipango yake ikiwemo sababu za kumchagua kocha Juma Mwambusi kuwa msaidizi wake.

Hans amesema moja ya mpango wake mkubwa ni kuhakikisha Azam FC inafika mbali zaidi, kuanzia kupata ubingwa wa michuano ya ndani kama Ligi kuu na Kombe la Shirikisho pia kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.

Kocha huyo raia wa Uhalanzi ameelezea sababu za kumchagua Kocha Juma Mwambusi kuwa msaidizi wake, akisema hajaona maana yoyote ya kumtafuta kocha kutoka nje wakati anatambua uwezo wa Mwambusi na anaamini atamsaidi kutimiza mipango yake ndani ya Azam FC.

Naye Meneja wa Azam FC Philip Alando amesema kuwa katika mkataba waliokwisha saini na Hans hawajaweka masharti yoyote kama wafanyavyo vilabu vingine vikimtaka kocha asipofanya jambo kwenye timu wanamfukuza.

Kocha Hans ambaye amewasili nchini siku nne zilizopita akitokea Ghana kwa mapumziko amesema jana alikutana na wachezaji wote na kuwaeleza mambo anayoyahitaji kwaajili ya kufikia malengo ikiwemo nidhamu na kujituma huku pia akiweka wazi kuwa hatoangalia jina la mchezaji bali uwezo na kujituma.K
Theme images by rion819. Powered by Blogger.