HEAMEDA MEDICAL CLINIC ILIYOPO BUNJU B YATANGAZA KAMPENI YA KUPIMA AFYA KWA WANANCHI BURE


HEAMEDA Medical Clinic iliyopo Bunju B njia ya kuelekea Mabwepande imetangaza kambi ya uchunguzi wa afya ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wote na kwamba hakutakuwa na gharama.

Akizungumza na leo jijini Dar es Salaam Dk. Hery Mwandolela amesema wameaza kambi hiyo ya uchunguzi jijini Dar es Salaam kwa kupima wananchi mbalimbali waliojitokeza na kusisitiza upimaji huo ambao umeanza Julai 26 utaendelea hadi Julai 28 mwaka huu.

Amesema upimaji huo unafanywa na Madaktari bingwa wa hapa nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchini India na lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kutambua afya zao mapema na iwapo watabainika kuwa na tatizo la kiafya waaze tiba mapema.

Amefafanua huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ya uchunguzi ni pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya Moyo ,sukari,shinikizo la damu,Tenzi Dume, lehemu(cholestrol) nakiwango cha mafuta mwilini."Madaktari bingwa wa Heameda Medical Clinic kwa kushirikiana na madaktari bingwa wengine nchini pamoja na madaktari bingwa kutoka India tutatoa huduma hizo kwa kiwango cha hali ya juu.

"Hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi nakwamba huduma hii inafanyika kwa siku tatu ambapo tumeaza leo na tunaendelea kesho na keshokutwa na hakuna gharama yeyote ."amesema Dkt Mwandolela.

Amesisitiza kwakutambua umuhimu wa afya yako wameamua kufanya kampeni hiyo ya kupima magonjwa hayo wakiamini ni fursa ya kila mwananchi kujitambua kiafya mapema.

Katika kampeni hiyo kwa siku ya leo ambayo ni ya kwaza idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza lakini Dkt.Mwandolela anafafanua kwa idadi ya madaktari bingwa waliopo nivema wananchi wakaendelea kujitokeza kwani wote watahudumiwa kwakupata vipimo vya afya zao.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Dk.Hery Mwandolewa akiwa ofisini kwake Heameda Medical Clinic Bunju B jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa sehemu ya mapokezi ndani ya Clinic hiyo
Muonekano wa moja ya chumba chenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa/matibabu
Muoneakano wa Clinic hiyo kwa nje

Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527