Friday, July 27, 2018

WANAFUNZI WASHINDWA KUTUMIA VYOO

  Malunde       Friday, July 27, 2018

Picha kwa hisani ya mitandao, haihusiani na habari husika.

Wanafunzi wa shule ya msingi Maleshi, Kijiji cha Endadoshi wilaya ya Babati mkoani Manyara wametajwa kuwa hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa maji ya kutumia katika vyoo vya kisasa vilivyopo shuleni hapo.

Imeelezwa kwamba kutokana na ukosefu wa maji ndani ya kijiji hicho imewalazimu wanafunzi wa shule hiyo ambao wengi wapo darasa la awali, na la kwanza kutumia choo ambacho ni hatari kwa maisha wanafunzi hao, kutokana na kujaa kwa kinyesi kwenye matundu ya vyoo hivyo vya kisasa.

Kwa mujibu wa wanakijiji kutoka ndani ya eneo hilo wameeleza kuwa hali ya watoto wao ipo mashakani kwa kuwa hawawezi kuwapa watoto wao maji ya kupeleka shuleni ikiwa wao wenyewe majumbani hawana maji ya kutumia.

"Wananchi pia maji hatuna, matumizi ya nyumbani ukujumlishia na hiyo shule utawapa watoto nini? watoto wanakwenda bila kuoga shuleni kutokana kwamba maji hakuna kabisa. Serikali iliyopo madarakani tunaomba itusaidie hapa tulipo" amesema mmoja wa wanakijiji.

Naye Msimamizi wa shule hiyo Jacob Mwenda amesema kuwa tofauti na wanafunzi kuhatarisha maisha yao, pia wanafunzi wengi huenda shuleni bila ya kuoga kitu ambacho kinawafanya muda wote kujikuna na kushindwa kuwa makini wakati wa ufundishwaji.

Mwaka huu aliyekuwa Waziri wa Maji, Dkt. Issack Kamwelwe kabla hajahamishwa wizara aliwasilisha amewasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2018/19 ya Sh727.35 bilioni ikiwa na ongezeko la zaidi ya Sh79 bilioni ukilingasha na bajeti ya mwaka 2017/18 ya Sh648.01 bilioni.

Akiwasilisha bajeti hiyo Mei 7, 2018, bungeni mjini Dodoma, Waziri Kamwelwe alisema kati ya fedha hizo Sh697.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya sekta ya maji.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post