MBUNGE WA CHADEMA AHAMIA CCM

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM leo Jumamosi Julai 28, 2018.


Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.


Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.


Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM. Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).
Theme images by rion819. Powered by Blogger.