Friday, July 6, 2018

LIPULI FC YAUA NDEGE WANNE KWA JIWE MOJA

  Malunde       Friday, July 6, 2018
Katika kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2018/19 wa Ligi kuu soka Tanzania Bara, Klabu ya soka ya Lipuli FC imenasa sahihi za wachezaji wanne kwa siku moja akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Yanga Paul Nonga.
Mchezaji Paul Nonga akiwa ndani ya ofisi za Lipuli FC baada ya kusaini mkataba.

Lipuli FC imemsajili mlinzi mahiri wa zamani wa Simba, ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea klabu ya Ndanda FC ya Mtwara William Lucian kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mbali na Lucian, mshambuliaji Paul Nonga ambaye alikuwa anaichezea Mwadui FC msimu uliopita, naye amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Lipuli FC pia kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kushoto ni mchezaji William Lucian akiwa na kiongozi wa Lipuli FC na kulia ni Miraji Madenge akiwa ameshikilia jezi ya Lipuli FC.

Lipuli FC pia imewasajili mshambuliaji Issa Ally Rashidi akiwa kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na Miraji Madenge ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea MWADUI FC.

Mchezaji Issa Ally Rashidi (kushoto) baada ya kusaini mkataba na Lipuli FC.

Lipuli FC inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa Simba Suleiman Matola, ilifanya vizuri msimu uliopita na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya 7 ikiwa ndio msimu wake kwanza kurejea ligi kuu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post