WAZIRI NDALICHAKO : MARIA NA CONSOLATA NI MASHUJAA WA TAIFA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa Mapacha walioungana Maria na Consolata mkoani Iringa ambapo alizungumza na waandishi wa habari na kusema mapacha hao Maria na Consolata ni mashujaa wa Taifa na kwamba wameliacha taifa katika simanzi nzito.

"Mara ya mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.

Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.