PERU WAVUNJA REKODI YA MIAKA 40 KOMBE LA DUNIA


Mfungaji wa bao la pili la Peru Paolo Guerrero

Timu ya taifa ya Peru imemaliza mechi zake za makundi kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Australia na kuvunja rekodi yake ya kutoshinda mchezo kwenye Kombe la Dunia tangu mwaka 1978.

Tangu ishinde mechi yake ya mwisho dhidi ya Iran kwa mabao 4-1, imepita miaka 40 na siku 15. Ushindi wa Peru leo haujaisaidia kusonga mbele ambapo imetoka pamoja na timu ya Australia.

Katika kundi hilo la C timu ya Ufaransa imeongoza ikiwa na alama 7 ikifuatiwa na Denmark yenye alama 5. Ufaransa itasubiri mshindi wa pili wa Kundi D huku Denmark ikiwa inasubiri mshindi wa kwanza ambapo Croatia ina nafasi kubwa ya kuongoza kundi hilo.

Pia mechi kati ya Ufaransa na Denmark imekuwa mechi ya kwanza kumalizika kwa suluhu kwenye Fainali za Mwaka huu. Naye kocha wa Ufaransa Didier Deschamps ameifikia rekodi ya kocha wa zamani wa Raymond Domenech ya kufundisha kwa mechi 79.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.